Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana
Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwa niaba ya Waziri Wizara ya
Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara katika meza kuu wakati wa
maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa Duniani ambapo Tanzania iliadhimishwa
katika viwanja vya Temeke Mwembeyanga. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi.
Mariam Khan na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Bw. Festus Ilako.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan (kushoto)
akisalimia umati wa wakazi wa jijini Dar (hawapo pichani) na kutoa ujumbe kwa
vijana kuungana na kujiepusha na mangonjwa hatarishi. Kulia Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana
Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA
Bi. Mariam Khan.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt.
Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya
Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana kujitambua na kuwa na
mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili Serikali iweze kuwasaidia kupata
misaada na kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu katika siku hii ya
maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila
tarehe 11 Agosti na kutimiza malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere juu ya Vijana.
Umati wa wakazi wa Temeke katika tamasha la siku ya
maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambako zilifanyika shughuli mbambali
ikiwemo ujumbe kutoka Serikalini na Kupima virusi vya Ukimwi bure.
Baadhi ya Vijana wakitazama machapisho ya vijarida mbalimbali vinavyotoa taarifa kuhusiana na Afya zao na jinsi ya kupata huduma.
Mmoja wa wakazi wa jijini Dar es Salaam akicheki
Afya yake
Wakazi waliohamasika kupima VVU na magonjwa ya Zinaa
wakiwa katika foleni ya kupata huduma hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya vijana Duniani katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar
Kikundi cha Sarakasi cha Rayon Kids kutoka Temeke
kikitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment