Tuesday, August 14, 2012

RAIS DKT. KIKWETE AWASILI KUTOKA GHANA, AFUTURU NA WATOTO YATIMA NA WALEMAVU IKULU


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik muda mfupi baada ya kuwasili akitokea nchini Ghana ambapo alishiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Atta Mills.




Baadhi ya watoto yatima na walemavu wakishiriki katika futari ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.





Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisoma barua aliyoandikiwa na mtoto Khaitham Jumbe (kulia) wakati wa futari aliyowaandalia watoto walemavu na yatima ikulu jijini Dar es Salaam.Katikati anayeangalia ni mtoto Hamida Jacks mdogo wake Khaitham.Mtoto Khaitham Jumbe ni mlemavu wa ngozi na alikuja ikulu na wazazi wake.




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakigawa zawadi kwa watoto yatima na walemavu walohudhuria futari waliyowaandalia ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni

_________________

For more information, comments,
please contact:

E-mail: thpi2009@gmail.com



No comments:

Post a Comment