Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Precision Air Bw. Alfonse Kioko
akizungumza na wageni na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla
ya kutiliana saini na Taasisi binafsi ya Tumaini la Maisha ambapo amesema kuwa
taifa lenye afya ndio lenye uwezo wa kupata maendeleo na kuongeza kuwa watoto
wanahitaji uangalizi na huduma bora za afya ili kujenga taifa lenye afya bora
na mafanikio siku za usoni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Tumaini la
Maisha Bi. Blandina Lugendo na kulia ni Daktari Bingwa wa Saratani za Watoto (Paediatric Oncologist) Dkt. Trish
Scalan.
Bw. Alfonse Kioko wa Precision air wakitiliana saini mkataba na Bi.
Blandina Lugendo wa Taasisi ya Tumaini la Maisha, utakaoshuhudia kampuni ya
Precision Air ikitoa tiketi za ndege kwa Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania,
ambazo zitatumika kusafirisha watoto wenye saratani pamoja na wazazi au walezi
wao kutoka jijini Dar es Salaam kwenda sehemu mbalimbali nchini.
Wakikabidhiana
mkataba wa makubaliano hayo.
Kampuni ya huduma za usafirishaji wa anga ya Precision Air imeingia
katika ubia na taasisi binafsi ya Tumaini la Maisha Tanzania ambayo
inajihusisha na kuboresha maisha ya watoto wenye saratani nchini Tanzania.
Kampuni hiyo itakuwa ikitoa tiketi mbili zilizolipiwa ushuru kwa mwezi na
kuwezesha kusafirisha wagonjwa kwenda katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza katika hafla ya kusain imkataba wa ubiahuo, Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya Precision Air Bw. Alfonse Kioko amesema wanayo furaha kuingia
katika ushirikiano huo katika jitihada za kujenga taifa lenye afya.
Bw. Kioko ameongoza kusema kuwa
wapo maelfu ya watoto wanaosumbuliwa na saratani ndani ya nchi yetu, na ni
lengo lao sasa kuhakikisha tunawarahisishia ugumu wa maisha katika kupambana na
ugonjwa huo.
Taasisi ya Tumaini la Maisha Tanzania imekuwa taasisi ya kwanza ya
kijamii yenye dhamira ya kuboresha afya za watoto waishio na ugonjwa wa
saratani nchini Tanzania.
Moja ya malengo ya Taasisi hiyo ni pamoja na kujenga wodi mpya ya
Saratani katika hospitali ya taifa Muhimbili ili kuweza kutoa huduma kwa watoto
na familia zao na kuepuka wingi wa wagonjwa katika wodi za hospitali hiyo.
SOURCE: www.dewjiblog.com
________________
Media Contact:
E-mail: thpi2009@gmail.com
No comments:
Post a Comment