Friday, March 30, 2012

PRESS RELEASE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMPENI YA KUCHANGISHA DAMU KUSAIDIA MAMA WAJAWAZITO WENYE UPUNGUFU WA DAMU WAJIFUNGUE SALAMA, AWAMU YA KWANZA

Taasisi ya madaktari wahitimu vyuo vikuu vya Tanzania, Tanzania Health Promotion Initiative (THPI) kwa heshima na taadhima wanayo furaha kubwa kuujulisha umma wa Tanzania kwamba tarehe 31/03/2012 Jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 7 mchana tutaendesha zoezi la kuhamasisha taifa kuchangia damu.

Lengo ni kuhamasisha wa Tanzania kujenga utaratibu wa kwenda kuchangia damu mara kwa mara kadiri inavyoshauriwa ili kuwa na damu ya kutosha katika vituo vyetu. Ikiwa ni jitihada ya kuokoa maisha wakina mama wajawazito wanaopata matatizo ya upungufu wa damu wakati wa ujauzito, kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua.

Kuna upungufu mkubwa wa damu katika hospitali zetu hivyo wananchi tujenge tabia ya kuchangia damu ili kuondoa tatizo hili.

Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu kuu ya “Saidia mama mjamzito ajifungue salama” ambayo ni kampeni ya kitaifa inayolenga kuhamasisha taifa kutekeleza malengo ya millennia lengo la 4 na la 5 ya kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na maendeleo.

Shukrani kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara kwa kusaidia kufanikisha maandalizi ya kampeni hii.
Tunashukuru taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kutupa ushirikiano madaktari vijana katika kampeni hii.

Wito kwa serikali iendelee kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuongeza ufanisi katika kupunza vifo vya mama na watoto. Kwa vyombo vya habari kusaidia kuelimisha na kuhamasisha umma kujielekeza kusaidia mama wajawazito wajifungue salama. Kwa wananchi tunaomba muitikio wao katika kuchangia damu ili kusaidia mama wajawazito wenye upungufu wa damu. Tunatoa rai kwa wahisani kuongeza nguvu ya kifedha kufanikisha kampeni hii.

Imetolewa na:

Dkt. Elisia Mpango

Katibu Mkuu

Tanzania Health Promotion Initiative - THPI

No comments:

Post a Comment