Tuesday, March 27, 2012

KAMPENI YA KITAIFA JUU YA UHAMASISHAJI WA UCHANGIAJI DAMU KUOKOA MAISHA YA MAMA WAJAWAZITO WANAOHITAJI DAMU.

THPI
TANZANIA HEALTH PROMOTION INITIATIVE
( Taasisi ya Madaktari Wahitimu Vyuo Vikuu Vya Tanzania)


Kwa Kushirikiana na

Kitengo Cha Damu Salama Cha Taifa na Kitengo Cha Damu Salama Kanda ya Pwani.


KAMPENI YA KITAIFA JUU YA UHAMASISHAJI WA UCHANGIAJI DAMU KUOKOA MAISHA YA MAMA WAJAWAZITO WANAOHITAJI DAMU, AWAMU YA KWANZA.


Kauli Mbiu: Jiwekee Utaratibu wa Kuchangia Damu, Okoa Maisha ya Mama Mjamzito

Lengo: Kukusanya Damu kwa ajili ya Kusaidia mama wajawazito Hospitali za Temeke,
Amana, Mwananyamala na Muhimbili.

Kampeni Kuu: Saidia Mama Mjamzito Ajifungue Salama.


Mahali: Viwanja Vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam.

Muda: Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 7:00 Mchana

Tarehe: Jumamosi Tarehe 31/03/2012

Mgeni Rasmi: Mama Salma Kikwete- Mwenyekiti Taasisi ya Wanawake na Maendeleo- WAMA.

Utangulizi.

Kuelekea mwaka 2015, nchi nyingi Duniani zinaelekeza jitihada na nguvu zao katika kufika malengo ya milenia, hasa lengo la 4 na 5, kupunguza vifo vya mama na motto. Ni nchi 21 Duniani zilizo katika mwelekeo sahihi wa kufikia malengo ya millennia kuelekea mwaka 2015.

Takribani wakinamama 368,000 duniani wanapoteza maisha kutokana na ujauzito. Taarifa za dunia zinaonyesha kuwa wakina mama wajawazito walio katika nchi zenye idadi kubwa ya vifo vya mama na mtoto wako katika hatari ya kupoteza maisha mara 100 zaidi kulinganisha na nchi ambapo idadi ya vifo vya mama na mtoto ni ndogo.

Kwa upande wa Tanzania vifo vya mama na mtoto vimepungua kutoka 578/100000 kwa mwaka 2005 hadi 454/100000 kwa takwimu za mwaka 2010. Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa upande wa Tanzania UNDP-Tanzania linasema pamoja na kushuka kwa idadi ya vifo, bado changamoto ni kubwa sana.

Wakina mama wengi wajawazito wanapoteza maisha kutokana na kukosa damu, wengine wanamatatizo ya kupoteza damu wakati wa ujauzito (anaemia in pregnancy) kabla ya kujifungua(Ante-partum haemorrhage), baada ya kujifungua (Post-partum haemorrhage). Mara nyingi maabara zetu hazina damu za kutosha kila wakati kusaidia mama wajawazito wenye matatizo ya damu, mara nyingi wanapelekwa hospitali za rufaa na wengi wanakufa njiani.

Hivyo basi Taasisi ya Madaktari Wahitimu Vyuo Vikuu Vya Tanzania, Tanzania Health Promotion Initiative, THPI, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendesha kampeni ya hamasa ya Kitaifa ili kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kujipangia utaratibu wa kwenda katika vituo vyetu vya afya ili kuchangia damu.

Lakini pia zoezi la uchangiaji damu ni kuendeleza kampeni ya kitaifa ya “Saidia Mama Mjamzito Ajifungue Salama”.

Washiriki

A. Viogozi wa serikali

1.Mh. Dr. Fenella E. Mukangara (MB) – Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo.
2.Mh. Mary Nagu (MB) Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji
3.Mh. Amina Makilagi Mbunge na Katibu Mkuu wa Umoja Wa Wakina Mama Tanzania.
4.Mh. Meck Sadik Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
5.Mh. Anjela Kairuki- Mbunge. Makamu mwenyekiti kamati ya sheria ya bunge.
6.Mh. Jordan Rugimbana- DC Kinondoni.
7.Mh. Halima Mdee-Mbunge
8.Mh. Idd Azan – Mbunge
9.Mh. Abasi Mtemvu-Mbunge
10.Mh. Dr.Faustine Ndungulile-Mbunge
11.Mh. Magreth Sitta- MBunge na Mwenyekiti wa Kamati ya huduma ya jamii ya Bunge.
12. Stara Thomas - Balozi wa Mama na Mtoto

B.Taasisi na Makampuni.

1.Wawakilishi wa Vyombo Vya Ulinzi ( Jeshi la Polisi, JWTZ, JKT )
2. Wawakilishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania, UWT.
3.Wawakilishi Chama Cha Madaktari Tanzania.
4.Wawakilishi MEWATA,
5.Wawakilishi NMB
6.Wawakilishi Tanzania Women Bank,
7.Wawakilishi Airtel,
8.Wawakilishi Diamond Trust Bank,
9.Wawakilishi NSSF,
10.Wawakilishi PSPF
11.Wawakilishi IPP Media, TBC1, Star TV, Mwananchi, Uhuru Publications etc.
12.Wawakilishi chama cha waandishi wa habari za michezo,Tanzania
13.Vijana,Wakina mama na Kina baba, Temeke, Kinondoni na Ilala.
14.Wanafunzi vyuo vikuu, Sekondari

C.Burudani.
Itatolewa na Msondo Music Band na Balozi wa Mama na Mtoto Stara Thomas.

D.Wito Kwa Wananchi.
Wananchi wote mnaombwa kuhudhuria kwa wingi kuja kuchangia damu ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito wanaohitaji damu.

E.Motisha.
Kwa yoyote atakaechangia damu kutakuwa na zawadi ya T-Shirt ya THPI na soda na atatambuliwa na damu salama kama mwanachama.

Ratiba

Na. Muda (Asubuhi) Tukio Mhusika
1. Saa 03:00-03:30 Kuwasili Wote

2. Saa 03:30-04:30 Kuwasili Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti WAMA

3. Saa 04:30-05:00 Burudani Msondo Music Band

4. Saa 05:00- 05:10 Utambulisho na Utangulizi Katibu Mkuu THPI, Dr. Elisia Mpango

5. Saa 05:10-05:20 Ufafanuzi juu ya Kampeni ya Saidia Mama Mjamzito ajifungue salama Mratibu Taifa Mama na Mtoto THPI, Dr. Jubilate Msangi

6. Saa 05:20-05:30 Malengo ya Kuchangisha Damu Grace Maliva Mkurugenzi Masuala ya Damu - THPI

6. Saa 05:30-05:45 Hali halisi ya vifo vya kina mama wajawazito kitaifa na Duniani. Mkurugenzi Mtendaji THPI, Dr. Telesphory Kyaruzi

7. Saa 05:45-05:50 Burudani Stara Thomasi

8 Saa 05:50-06:10 Salaam kutoka Mkurugenzi Damu Salama Taifa Mkurugenzi Damu Salama

9 Saa 06:10-06:15 Salaam kutoka kwa viogozi mbalimbali Viongozi
Burudani Msondo Music Band

10 Saa 06:15-06:20 Salaam Kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Meck Sadic

12 Saa 06:30-06:35 Hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete- Mwenyekiti WAMA.

13 Saa 06:35-06:45 Shukrani Mwakilishi Chama Cha Wachangiaji Damu Tanzania

14 Saa 06:45-07:00 Burudani Msondo Music Band

No comments:

Post a Comment