Tuesday, May 15, 2012

WAHITIMU VYUO VIKUU TUMIENI TAALUMA YENU KUTENGENEZA AJIRA




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk. Mary Nagu (MB) amewataka wahitimu wa vyuo vikuu katika fani mbalimbali hapa nchini kutumia elimu na utaalamu wanaoupata katika vyuo  mbalimbali hapa nchini  kwa kuweka mipango madhubuti ya kujiajiri.

Nagu aliyasema hayo wakati alipoongoza  matembezi ya “SAIDIA  MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA SALAMA” yaliyoandaliwa na Taasisi ya Madaktari wahitimu wa Vyuo Vikuu Tanzania (THPI) yaliyoanzia katika hospitali ya Manispaa ya Temeke mpaka Ofisi za Manisipaa ya hiyo, Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari 2012.

“Kwa niaba ya serikali napenda kuwapongeza Taasisi ya Madaktari Wahitimu wa Vyuo Vikuu Tanzania kwa kuwa chachu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika  kuwezesha vijana kujiajiri na napenda kuwahakikishia kuwa serikali inatambua mchango wenu wa kuunga mkono serikali katika kuboresha huduma za afya kwa akina mama na watoto” alisema Nagu

Aliongeza kuwa maendeleo ya elimu  nchini ya mechochea kuongezeka kwa vyuo vikuu hapa nchini na idadi ya wahitimu katika vyuo hivyo , ikiwa ni ishara ya uthubutu na utayari wa serikali katika kuwekeza na kusimamia sekta ya elimu hapa nchini lakini bado idadi ndogo ya wahitimu wanaoweza kupata ajira  katika sekta ya umma na binafsi kutokana na ufinyu wa nafasi hizo.

Aidha  Nagu alifafanua kuwa pamoja na kuwa Taasisi hiyo kuwa  inatengeneza ajira kwa vijana jambo kubwa  inalolitekeleza vizuri ni kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha afya ya Mama mjamzito hapa nchini ,mpango wenye lengo la kupunguza  vifo kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga.

Awali akimkaribisha Nagu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Madaktari Wahitimu Vyuo vikuu Tanzania,  Dk. Telesphory Kyaruzi alieleza kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni jinsi ya kuwapelekea huduma wanachi kwa wakati na kwa gharama wanazoweza kuzimudu.

Dr. Kyaruzi albainisha kuwa ukubwa wa changamoto huo pia unatokana na jinsi ya kuwafikia wananchi na hasa akina mama.

Katika mwaka 2010 kumekuwa na mafanikio makubwa katika kupungua kwa vifo vya mama wajawazito na wototo kufikia 454 kati ya watoto hai 100,000 kutoka 578 kwa mwaka 2005.



No comments:

Post a Comment